Thursday, October 20, 2016

Juma Muhamed Khamis
Tanzania

Imelezwa kuwa uwepo wa sera na sheria zisizotoa mwanya kwa wananchi wa hali ya chini Nchini Tanzania ni miongoni mwa sababau zinazowafanya wananchi hao kuendelea kuishi maisha duni licha ya rasilimali zao waliozonazo.

Hayo yamesemwa na mtalamu wa maswala ya gesi Nchini Tanzania Neema K.Lugangira wakati alipokuwa akitoa maelekezo kwa waandishi wa haabari wanaoendelea kupatiwa mafunzo ya rasilimali gesi na mafuta katika ukumbi wa white sand hotel jijini Dar es Salam.

Alisema uwepo wa sera hizo na sharia mbazo kwa namna moja au nyengine zinaonekana kuwabana wananchi wa Tanzania iwapo wanataka kuekeza katika secta ya rasilimali zao.

Akitaja miongoni mwa sababu nyengine ambazo zinawazuia wananchi wa Tanzania kutoweza kuwekeza katika rasilimali nikutokana kuwa na mtaji mdoogo wa kifedha jambo ambalo ni changamoto kubwa kwao ukizingatia secta hio inahitaji fedha nyingi sana ili uweze kuwekeza.

‘’Nafkiria moja miongoni mwa changamoto zinazowakabili wananchi wa kawaid Nchini Tanzania kuhusiana na rasilimali zao ni ukosefu wa mipango bora pamoja na rasilimali fedha ’’alisema mtalamu huyo.

Mafunzo hayo ya wiki mbili kwa waandishi wa habari yanayoendelea Nchini Tanzania yamewakutanisha baadhi ya wanahabri kutoka Uganda Tanzani pamoja na Ghana huku washiriki.
 

No comments:

Post a Comment